• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CMG yaandaa tamasha kwa ajili ya kusherehekea mwaka mpya wa jadi wa kichina

    (GMT+08:00) 2019-02-04 20:57:19

    Leo tarehe nne ni mkesha wa mwaka mpya wa jadi wa kichina. Shirika kuu la Utangazaji la China CMG limeandaa tamasha maalumu kuusherehekea.

    Tamasha hilo lenye kauli mbiu ya "kujiendeleza katika zama mpya, na kusherehekea mwaka mpya wenye baraka" litatangazwa saa mbili usiku wa leo. Likiwa tamasha la kwanza tangu CMG izinduliwe, tamasha hilo litakuwa na maonesho mazuri ya nyimbo, ngoma, opera za kichina, michezo mifupi ya kuigiza na mazungumzo ya kuchekesha.

    Mwaka huu tamasha hilo litaoneshwa kwa mara ya kwanza kupitia majukwaa mbalimbali, ikiwemo televisheni, radio, APP na mitandao ya kijamii, na teknolojia ya 5G pia itatumiwa kwa mara ya kwanza.

    Tangu mwaka 1983, kutazama tamasha hilo kumekuwa shughuli isiyokoseka ya wachina katika mkesha wa mwaka mpya wa jadi wa kichina.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako