• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wanafunzi wa taasisi wa confucious cho cha Kenyatta wakaribisha mwapa mpya wa kichina

  (GMT+08:00) 2019-02-05 08:46:28

  Taasisi ya kufunza kichina katika chuo kikuu cha Kenyatta nchini Kenya, imejiunga na Mamilioni ya wachina kusherehekea mwaka mpya wa kichina.

  Taasisi hiyo imeandaa manyesho ya densi, taichi na mapishi ya jaozi ili kusherehekea mwaka mpya.

  Hapa ni katika chuo kukii cha Kenyatta na wanafunzi pamoja na walimu wa taasisi ya Confucious wanafanya maonyesho ya kusherekea mwaka mpya wa kichina.

   

  Mwaka wa nguruwe.

  Na sio tu wanafunzi wa taaasisi hii lakini pia na wageni waalikwa kutoka shule za msingi ambako pia wanasoma lugha ya kichina.

  Leo pia wanafunzi wameonyesha weledi wao wa kuandika maandisi ya kichina.

  Siku hizi wanaifahamu fika sherehe ya mwaka mpya wa kichina kama vile Faith Shakutsa.

  "Kulingana na wachina, siku hii huwa ni kila mtu anarudi kwao nyumbani akae na wazazi wake kwa sababu wakati mwingi wanatoka nyumbani wanaenda mjini kufanya kazi, na hivyo mwaka mpya ni wakati kila mtu lazima aurdi kwao nyumbani. Chakula ya kichina ninachokipenda zaidi ni Hotpot"

  Naye Winfred Kawira anapenda tambi na jaozi.

  Akiwa kwenye taasisi ya confucious amekuwa akijifunza taichi na michezo mingine ya kichina.

  "Najifunza mazoezi ya sanaa za kichina kwa sababu zinasaidia mwili wangu. Nimekuwa nikipenda sanaa hii tangu kitambo, nilikuwa nawaona wachina wakifanya hivyo kwenye runinga. Napenda chakula chao hasa jaozi na tambi. "

  Umaarufu wa lugha na utamaduni wa China umeendelea kukua duniani kote kufuatia utambuzi unaoongezeka wa jukumu muhimu China inatekeleza kimataifa. Hivyo kuanzishwa kwa Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Kenyatta ni mojawepo wa uendelezaji wa lugha hiyo.

  Tangu kuanzishwa kwake Desemba 2008, Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Kenyatta imeendelea kukua na kuboresha programu za lugha za Kichina. Kumekuwa na ongezeko la idadi ya wanafunzi wanaojifunza Kichina hadi zaidi ya 3,000; na kuunganisha wahitimu wa Taasisi na mashirika yenye nia ya kuwaajiri wafanyakazi wenye ujuzi katika lugha ya Kichina.

  Profesa Li Jing mkuu wa taasisi ya Confucius hapa

  "Taasisi hii inaendeleza na kufunza lugha na utamaduni wa China na kuchangia ubadilishanaji wa utamaduni fursa na elimu. Kila mwaka mpya wa kichina tunaandaa halfa kama hii ili ili kusherehekea mpja na wanafunzi wetu na waalimu. Tunawaalika wageni wengine. Hii pia ni fursa zuri ya kuonyesha masomo tunayofunza na jinsi wanafunzi wanasoma"

  Ushirikiano wa mafunzo ya kichina kwenye chuo hiki umepata maendeleo mapya baada ya serikali ya china kugharamia ujenzi wa jumba la utamaduni na lugha kwa gharama ya shilingi bilioni 1.2.

  Na mkurungezi wa taasisi hii bwana Kamau Wango, anasema mwaka hadi mwaka wanafunzi wameendelea kupata msaada wa kimasomo kuendeleza elimu yao nchini China.

  "Taasisi ya Confucius intakuwa kwenye sehemu moja ya hilo jengo. Imefadhiliwa na serikali ya China na sasa imekabidhiwa chuo kikuu cha Kenyatta na iko na vifaa vingi sana ambazo zitatusaidia kufunza lugha na tamaduni za kichina. Mwaka huu tutapeana msaada kwa wanafuzni 30 hivi lakini ni lazima wahitumu kwanza "

  Huku mamilioni ya watu duniani wakisherekea mwaka wa kichina, mizizi ya urafiki wa jadi kati ya China na nchi nyingine imeendelea kuota hata zaidi, na sasa inatekeleza wajibu muhimu katika kukuza ushirikiano kwa njia ya kulinda amani, utoaji wa misaada ya elimu na miundo mbinu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako