• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Xi Jinping anakumbuka maisha ya wananchi Ndoto ya China waliyonayo wanakijiji

    (GMT+08:00) 2019-02-05 08:49:31
    Liang Jia He ni kijiji kidogo kilichoko kwenye Uwanda wa Juu wa kaskazini magharibi mwa China. Rais Xi Jinping amewahi kuishi na kufanya kazi kijijini hapo alipokuwa na umri wa miaka 15 hadi miaka 22. Katika muda huo wa ujana wake, alijionea hali halisi ya vijijini nchini China, ambapo hali halisi ya wananchi mashinani na matakwa yao vilimfanya awe na nia imara ya kufanya mambo halisi kwa ajili ya wananchi katika maisha yake yote. Katika kipindi hiki cha "Xi Jinping anakumbuka maisha ya wananchi", leo tunawaletea makala ya kwanza kuhusu "Ndoto ya China waliyonayo wanakijiji".

    Tarehe 22, Septemba, mwaka 2015, kwenye tafrija ya kumkaribisha aliyoandaliwa Rais Xi Jiping wa China alipokuwa ziarani nchini Marekani, aliwaeleza wamarekani akisema :

    "Mwishoni mwa miaka 60 ya karne iliyopita, nilipokuwa na umri wa miaka zaidi ya kumi tu, nilikwenda katika Kijiji cha Liang Jia He kutoka Beijing, nikaishi na kufanya kazi huko kwa muda wa miaka saba. Baadaye nilikuwa katibu wa Chama tawi la Liangjiahe, nikawaongoza wanakijiji kuongeza uzalishaji wa kilimo, ambapo nilitarajia sana kuona wanakijiji wanaweza kupata mlo hata mmoja wa nyama wa kushiba, na baadaye waweze kupata nyama mara kwa mara."

    Mwaka 1969, wanafunzi vijana wa China wapatao 17 akiwemo Xi Jinping aliyekuwa na miaka 15, waliitikia mwito wa taifa na kuondoka mijini na kwenda vijijini kushiriki kwenye kazi za kilimo. Baada ya kuishi na kufanya kazi kwa miaka saba kijijini, kijana Xi aliyetoka mji wa Beijing alibadilika kuwa kijana wa kijijini aliyekuwa na uwezo wa kufanya kazi ya kilimo. Mwanakijiji wa Liangjiahe Shi Chunyang mwenye miaka 63 alikumbusha hali ya wakati ule akisema:

    "wakati wa majira ya baridi, tulipofanya kazi ya kuzuia mmomonyoko wa ardhi, Xi Jinping alikuwa anafanya kazi pamoja nasi akiwa miguu peku bila kujali baridi kali na hatari kwa afya."

    Wakati Xi Jinping aliposoma habari kwenye gazeti kuhusu vijiji mkoani Sichuan kujenga mashimo ya kuzalisha gesi kwa kinyesi, alikwenda huko kujifunza, na baadaye aliwaongoza watu wa kijiji chake kujenga shimo la kwanza la kuzalisha gesi kwa kinyesi mkoani Shanxi.

    "tulikumbwa na taabu kubwa tulipojenga shimo la kwanza, baada ya kukamilisha kazi tuliona gesi ilikuwa haijaweza kutoka, tukatoboa shimo, mara kinyesi kiliruka hadi usoni mwangu, na gesi pia ilianza kutoka, tukafunga bomba mara moja, na moto uliwaka pia kwenye jiko."

    Xi Jinping aliishi kijijini, kujenga barabara na kujenga shimo la kuzalisha gesi kwa kinyesi, alijiunga na Chama cha Kikomunisti kijijini, baadaye akawa katibu wa tawi la chama la kijiji... maisha ya miaka saba kijijini yalimfanya akue vizuri na kuimarisha nia na imani. Katika makala moja akikumbusha maisha yake ya muda huo alisema:

    "Niliona nguvu ya umma, niliona hali halisi ya umma, niliwaelewa raia kihalisi, na hali ya jamii, huu ni msingi kabisa. Mawazo mengi yaliyotokana na mambo halisi yalianza kutia mizizi na kuchipuka kuanzia wakati ule, na mpaka sasa yananigusa kila dakika."

    Wakati wa mkesha wa Sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China wa 2015, Xi Jinping alirudi Kijiji cha Liangjiahe anachokumbuka sana moyoni, alikaribishwa kwa furaha na wanakijiji na kukutana na marafiki wengi walioishi na kufanya kazi pamoja. Xi Jinping alipokumbusha kuhusu safari yake hii alisema: "Kijiji sasa kina barabara ya lami, wanakijiji wanaishi katika nyumba za matofali, na kutumia mtandao wa internet, wazee wamepata matunzo ya uzeeni ya kimsingi, wanakijiji wanashiriki kwenye bima ya matibabu, na watoto wanaweza kupata elimu nzuri, na kupata nyama sasa ni jambo la kawaida. Hivyo nimetambua kwa kina, Ndoto ya China ndiyo ndoto ya wananchi, ni lazima kuihusisha na matarajio ya wananchi wa China kuhusu maisha mazuri, ili tutimize Ndoto ya China?

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako