• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tamasha la Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China lafanyika

    (GMT+08:00) 2019-02-05 09:35:18

    Tamasha la kusherehekea mkesha wa Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China lilifanyika jana usiku.

    Tamasha hilo limeandaliwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, na kutumbuizwa kwa nyimbo, ngoma, mazungumzo ya kuchekesha, mazingaombwe na sarakasi ambazo zimeonesha imani thabiti ya watu kutafuta na kutimiza ndoto ya China, na kueleza furaha na hisia ya kupata waliyo nayo watu wa China.

    Tamasha hilo la mwaka huu ni la kwanza kufanyika baada ya kuzinduliwa kwa CMG, ambayo imetumia njia mbalimbali za vyombo vya habari na teknolojia mpya kama vile 4K, 5G, VR kulitangaza. Pia limeshirikiana na kampuni za Baidu na TikTok na kuchezesha bahati nasibu.

    Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China ni siku ya kujumuika kwa wanafamilia, ndiyo maana "familia", "upendo" na "neema" ni kauli mbiu muhimu ya tamasha hilo. Mwaka huu ni mwaka wa 70 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China na pia ni kipindi kipya cha kuelekea utimizaji wa jamii yenye maisha bora, hivyo tamasha hilo limeandaa mazingira mazuri ya kukaribisha maadhimisho hayo na mafanikio ya ujenzi wa jamii yenye maisha bora.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako