• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Xi Jinping anakumbuka maisha ya wananchi   Watu anaowakumbuka zaidi

    (GMT+08:00) 2019-02-06 09:10:29

    Kila inapokaribia Sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China, Rais Xi Jinping huwa anakwenda kutembelea sehemu zenye watu umaskini nchini China, kama alivyosema: "Wakati huo, ninawakumbuka zaidi watu wenye matatizo ya kiuchumi". Mpaka sasa karibu ametembelea karibu sehemu zote zenye ngumu ya umaskini, akikagua hali halisi ya watu wa huko, na kuchunguza sababu za kuwa nyuma kimaendeleo, ili kulenga kwa usahihi namna ya kuzisaidia zijiendeleze na kuondoa umaskini. Xi Jinping alisisitiza kuwa, kwenye njia ya "kujenga jamii yenye maisha bora kwa pande zote", haturuhusiwi kumwacha mtu hata mmoja kwenye umaskini, "Ni lazima kuwawezesha wakulima wengi zaidi wanufaike na matunda ya mageuzi na maendeleo". Katika kipindi hiki cha leo cha Xi Jinping anakumbusha maisha ya wananchi, tunawaletea makala ya pili ya "Watu anaowakumbuka zaidi."

    Xi Jinping: "Mwaka jana watu wangapi walioa?"

    Guo Jinaqun: "Watu saba." (Vicheko)

    Hayo ni maongezi kati ya Xi Jinping na Guo Jianqun, mkuu wa Jimbo linalojiendesha la makabila ya watujia na wamiao la kaskazini magharibi ya Mkoa wa Hunan katika wakati wa "Mikutano ya Bunge la Umma na Baraza la Mashauriano ya Kisiasa" ya China. Xi Jinping alimwuliza Bw. Guo kuhusu hali ya Kijiji cha Shi Ba Dong cha sehemu hiyo, na alifuatilia hali ya ndoa za wanakijiji, kihalisi alifuatilia sana maendeleo ya kazi ya kuwasaidia watu waondokane na umaskini. Kutokana umaskini, zamani kijijini humo vijana wengi wa kiume walishindwa kuoa. Mwezi Novemba mwaka 2013, Xi Jinping alifanya ukaguzi Kijijini Shi Ba Dong kilichoko mbali mlimani. Nyumbani kwa Bw. Shi Chiwen ambaye ni maskini zaidi, Xi Jinping aliwauliza mzee huyo na mke wake hali ya familia hiyo kuhusu uzalishaji na maisha.

    "Xi: Mnaweza kupata mchele wa kutosha?"

    Shi: Tunaweza kupata chakula cha kutosha.

    Xi: Mna pesa za matumizi? Mna kipato? Mnafuga mifugo?

    Shi: Tunafuga nguruwe wawili…"

    Kwenye kijiji cha Shi Ba Dong chenye watu chini ya elfu moja, wastani wa mapato ya kila mtu haukufika Yuan 1700 mwaka 2013, hata haujafikia moja ya tano ya ule wa mwanakijiji wa nchi nzima kwa wakati huo. Xi Jinping alipotembelea kijiji hicho alitoa agizo la "Kuwasaidia kihalisi watu wenye matatizo ya kiuchumi", akisisitiza kuwa, ni lazima kufanya kazi ya kuondoa umaskini kutokana na hali tofauti ya sehemu mbalimbali nchini, na kutoa maelekezo ya kazi za aina mbalimbali. Baadaye Kijiji cha Shi Ba Dong kiliweka mkazo katika kuendeleza uchumi wa kandarasi, upandaji wa mimea maalumu, ufugaji wa mifugo maalumu, utarizi maalumu wa kabila la wamiao, na shughuli za utalii na utoaji huduma, ambapo si kama tu kiliondoa umaskini mwaka 2017, bali pia kilitoa kielelezo kwa sehemu nyingine nchini. Na wakati wa kuondoa umaskini, wanaume wengi walifunga ndoa, na maisha ya mzee Shi Chiwen na mkewe pia yameboreshwa.

    Mwezi Juni mwaka 2017, Xi Jinping alifanya ukaguzi na utafiti katika sehemu ya mlimani ya Luliang mkoani Shanxi, ambapo alitembelea nyumbani kwa mwanakijiji Liu Fuyuo, Bw. Liu alisema:

    "Rais Xi aliniuliza kwa makini sana kuhusu matumizi yangu ya pesa, nilimwambia mbali na kununua mahitaji ya lazima ya maisha, asilimia 80 ya mapato yangu yalitumiwa kwa kununua dawa za matibabu."

    Kutokana na uchunguzi, idadi ya maskini kutokana na magonjwa, ilichukua zaidi ya asilimia 40 nchini China. Xi Jinping alidhihirisha kuwa ni lazima kuchukua hatua mbalimbali halisi, kuimarisha utaratibu wa bima ya matibabu na uhakikisho wa jumla, ili wagonjwa vijijini wajitoe kutoka kwenye janga la umaskini. Mwaka jana kati ya idadi ya watu maskini kutokana na matatizo ya ugonjwa, watu milioni 5.81 waliondokana na hali ya umaskini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako