• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjumbe wa China atoa mwito wa uungaji mkono katika kupambana na uhalifu baharini

    (GMT+08:00) 2019-02-06 09:40:20

    Mwakilishi maalumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Ma Zhaoxu ametoa mwito kwa nchi husika kutoa uungaji mkono katika kupambana na uhalifu wa baharini, na kusema kuwa usalama wa baharini bado unakabiliwa na changamoto kubwa katika pwani ya magharibi ya bara la Afrika.

    Balozi Ma amesema kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa China inaunga mkono nchi hizo katika kuimarisha uratibu, kupanga mikakati na mifumo ya pamoja, kupambana na uhalifu wa kupangwa wa kuvuka nchi unaofanyika baharini ili kutimiza maendeleo na mustakbali mzuri. Ameongeza kuwa katika miaka ya hivi karibuni, wakati mashambulizi ya uharamia katika Ghuba ya Aden yanapungua kidhahiri, hali ya usalama wa baharini katika Ghuba ya Guinea katika pwani ya magharibi mwa Afrika bado inakabiliwa na changamoto, ambayo inaathiri vibaya maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi za pwani barani Afrika.

    Ameonya kuwa pesa haramu zimeingia kwenye makundi ya kigaidi, makundi yenye itikadi kali, na makundi ya uhalifu, na kuzidisha hali ya utulivu wa kitaifa na kikanda kuwa mbaya, na kutishia amani na usalama wa kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako