• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: KRA yaomba kusaidia serikali za kaunti kukusanya ushuru

    (GMT+08:00) 2019-02-06 15:18:27

    Mamlaka ya ukusanyaji ushuru nchini Kenya KRA imesema iko tayari kusaidia serikali za kauti kukusanya kodi.

    KRA inasema ina miundo mbinu ya kutosha ambayo itasaidia serikali hizo kupata ushuru zaidi.

    Kamishena wa idara ya ushuru kwenye mamlaka hiyo Ruth Wachira, amesema ripoti ya hivi karibuni kwamba serikali nyingi za kaunti hazijatimiza malengo yao ya kukusanya ushuru, ni ishara kuwa hazina uwezo wa kutosha wa kufanya hivyo.

    Hata hivyo spika wa bunge la kaunti ya Nairobi, Beatrice Elachi amehoji kuwa huenda baadhi ya serikali hizo zinatangaza ukusanyaji mdogo ili kuendeleza ufisadi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako