• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa Kenya waonya mataifa ya nje kutoingilia mambo ya Afrika

    (GMT+08:00) 2019-02-06 18:54:39

    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameonya mataifa ya nje wasiingilie kati mambo ya ndani ya bara la Afrika. Kenyatta ameyasema hayo kwenye mkutano wake na makamu wa rais wa Sudan Osman Mohamed Yousif ambaye yuko kwenye ziara nchini Kenya.

    Baada ya kupokea salamu kutoka kwa rais wa Sudan Omar al-Bashir, Rais Kenyatta amesema Kenya na Sudan ni wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Serikali za Afrika Mashariki (IGAD), na ataendelea kushirikiana na Sudan kutatua changamoto zinazowakabili na kuwa kwa sasa hali imetulia nchini Sudan licha ya picha mbaya inayoelezwa na baadhi ya mataifa ya nje ya kutaka kuchafua bara la Afrika.

    Kwenye mkutano huo, makamu wa rais wa Sudan ameeleza Sudan inatambua umuhimu wa Kenya katika maendeleo ya nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako