• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa waeleza kupungua kwa vurugu nchini Sudan Kusini tangu makubaliano ya amani

    (GMT+08:00) 2019-02-06 19:00:52

    Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni kiongozi wa vikosi vya usalama vya umoja huo nchini Sudani Kusini David Shearer katika mkutano na wanahabari amesema, vurugu hususani za kisiasa zimepungua kwa kiasi kikubwa kusini mwa Sudan Kusini tangu kufikiwa kwa mazungumzo ya amani kati ya serikali ya nchi hiyo na upinzani mwezi Septemba mwaka jana.

    Shearer amesema, kumekuwa na hatua kubwa ya maendeleo nchini humo, na watu waliokimbia makazi yao kutokana na vurugu hizo wana matumaini makubwa ya kurejea majumbani.

    Hadi sasa karibu watu 130,000 wamesharejea nchini Sudan Kusini kutoka nchi jirani na karibu watu 193,000 wamepata hifadhi kwenye kambi za usalama wa raia kulinganisha na watu 205, 000 miezi mitano iliyopita.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako