• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WAMILIKI MATATU WAMSIHI SONKO ASIPUNGUZE ADA YA KUEGESHA MAGARI YA KIBINAFSI

    (GMT+08:00) 2019-02-07 18:58:44
    Wamiliki wa matatu jijini Nairobi wamesema msongamano unaoshuhudiwa husababishwa na magari ya kibinafsi.

    Serikali ya kitaifa kwa ushirikiano na ya kaunti ilikuwa imetangaza kuwa hakuna gari litakaloruhusiwa kuingia jijini Nairobi siku mbili kwa wiki, Jumatano na Jumamosi. Agizo hilo lilipaswa kuanza Jumamosi ya kesho lakini Waziri wa Uchukuzi James Macharia mapema wiki hii alisema limeahirishwa kwa muda.

    Kulingana na serikali ni kuwa pendekezo hilo la majaribio linapania kuondoa msongamano wa magari jijini Nairobi.

    Wamiliki wa matatu jijini wamesema msongamano unaoshuhudiwa husababishwa na magari ya kibinafsi.

    Kulingana na Jamal Mohamed, mwenyekiti wa muungano huo amesema changamoto za msongamano wa magari jijini Nairobi zitatuliwa iwapo magari ya kibinafsi yataondolewa katikati mwa jiji.

    Kwenye kikao na waandishi wa habari mapema Bw Jamal amemtaka Gavana Mike Sonko kufuta pendekezo lake la kushusha ada ya maegesho ya magari ya kibinafsi aliyotangaza kupunguza kutoka Sh300-200 mwezi Januari 2019. Mwenyekiti huyo amesema punguzo hilo la ada litachochea magari ya kibinafsi kufurika jijini Nairobi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako