• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mwakilishi wa Huawei akosoa shutuma za balozi wa Marekani na kutetea uadilifu na usalama

  (GMT+08:00) 2019-02-08 09:52:29

  Mwakilishi mwandamizi wa kampuni ya teknolojia ya China Huawei ametoa kauli kali pale aliposema kuwa hivi karibuni kampuni yake imekuwa ikishambuliwa na baadhi ya nchi na wanasiasa kwa shutuma zisizo na msingi wala maana, ambazo zimewashagaza na baadhi ya wakati kuwachekesha.

  Jana katika chumba kilichojaa wageni zaidi ya 100, wengi wao wakiwa ni watu wa Ulaya, Bw. Abraham Liu, naibu mkurugenzi wa kampuni ya Huawei katika kanda ya Ulaya na mwakilishi mkuu wa mashirika ya Umoja wa Ulaya alitoa mfano akisema Jumanne, balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Ulaya GordonSondland alisema kuna mtu aliyepo mjini Beijing ambaye aliendesha gari maalum lililoko huko barani Ulaya kwa mtandao wa 5G na kuiachanisha njia na kumwua mmoja aliyekuwemo ndani ya gari hilo. Amesema hii inadharau akili za watu, sembuse wataalam wa teknolojia kote duniani."

  Ameongeza kuwa kuondolewa Huawei sokoni hakumaanishi kuwa mtandao utakuwa salama, na kwamba kama vifaa vya Huawei havitumiki katika mitandao ya Marekani, haina maana Marekani ina mtandao salamu kabisa duniani. Amesema kampuni ya Huawei ina historia nzuri ya usalama mtandaoni, na vifaa vinavyoidhinishwa kwa upimaji mkali uliofanywa na idara na makampuni mbalimbali ya simu. Barani Ulaya, wenzi wa kampuni ya Huawei ni pamoja na Deutsche Telekom, British Telecom, Vodafone, Orange, Proximus na mengineyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako