• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uhamishwaji wa kodi ya majengo mfuko mkuu umeleta faida kubwa Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-02-08 18:37:31
    Waziri wa nchi,ofisi ya Rais,-Tawala za Mitaa (Tamisemi) ,Seleman Jafo,amesema kuondolewa kwa kodi ya majengo katika Mamlaka za serikali za Mitaa na kupeleka kwenye mfuko wa serikali kuu,kumesaidia mamlaka hizo kupata fedha za kutekeleza miradi zaidi ya mapato yaliyokuwa yanakusanya.

    Uchukuaji wa baadhi ya vyanzo vya mapato kwa mamlaka hizo ulifanyika kwa mujibu wa Sheria ya Bajeti ya Mwaka 2015 iliyoridhiwa na Bunge ,kodi ya majengo ikihamishiwa serikali kuu.

    Akizungumza na makatibu tawala wa mikoa,mameya wa majiji,na wenyeviti wa halmashauri waliopta fedha za ufadhili kwa ajili ya kutekeleza miradi miradi mikakati katika halmashauri 12 nchini humo,Jafo alisema uhamishaji huo ulikuwa na tija kwa kuwa sasa miradi inapelekewa zaidi zaidi ya makusanyo waliyokuwa wakitarajia.

    Waziri Jafo alisema lengo la serikali kufanya hivyo ni kuweka nidhamu ya ukusanyaji wa fedha ili zirudi katika mamlaka hizo kwenda kutatua matatizo ya wananchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako