• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Xi Jinping anakumbuka maisha ya wananchi   

  Katibu mkuu wa Chama azungumza kuhusu uvumbuzi

  (GMT+08:00) 2019-02-09 15:50:56

  Kufanya uvumbuzi ni kazi muhimu katika maendeleo ya China kwa zama tulizonazo. Katibu mkuu wa Chama Xi Jinping anasisitiza mara kwa mara kuwa, "Watu wanaofanya uvumbuzi ndio wanaoweza kupata maendeleo, nguvu na ushindi." Katika kipindi hiki cha Xi Jinping anakumbuka maisha ya wananchi, leo tunawaletea makala ya tano, kuhusu katibu mkuu wa Chama kuzungumzia uvumbuzi.

  "Leo mna furaha ? (sauti ya wengi): Tuna furaha!"

  Oktoba 22, 2018, Katibu Mkuu wa Chama Xi Jinping alitembelea Kampuni ya vyombo vya umeme nyumbani ya Gree, ambayo awali ilikuwa kiwanda kidogo cha viyoyozi nyumbani。Sasa kampuni hiyo imeendelezwa kuwa Kundi la viwanda la kimataifa, linalotengeneza vyombo vya umeme vya nyumbani Zana na vifaa vya hali ya juu na vya mawasiliano ya habari vinavyotengenezwa na kampuni hiyo vinauzwa katika nchi na sehemu zaidi ya 160 duniani, na siri ya maendeleo yake ni kushikilia kufanya uvumbuzi kwa kujitegemea.

  Xi Jinping aliwatia moyo wafanyakazi wa kampuni hiyo wawe na nia na ari kubwa ya kuharakisha kuongeza uwezo wa kufanya uvumbuzi kwa kujitegemea, na kushika mikononi mwao wenyewe haki ya kujiendeleza kwa kutegemea uvumbuzi. Akisema:

  "Nchi kubwa ikitaka kujiendelezwa kuwa nchi yenye nguvu, muhimu zaidi ni kutegemea thamani ya jumla ya bidhaa zinazozalishwa na nchi hii wakati wowote. Viwanda vya utengenezaji vinafanya kazi muhimu katika maendeleo ya bidhaa zenye thamani zinazozalishwa, na kiini cha viwanda vya utengenezaji ni kufanya uvumbuzi, yaani kuwa na teknolojia muhimu, hivyo ni lazima kufanya uvumbuzi kwa kujitegemea, na viwanda vyote vinatakiwa kufanya juhudi zaidi kuelekea mwelekeo huu."

  Wafanyakzi wengi: "Tunaahidi kufanya juhudi mara dufu, ili dunia ipende bidhaa zinazotengenezwa na China."

  Mwezi Juni, 2018, Xi Jinping alitembelea Kituo cha kutengenza kompyuta za hali ya juu cha kampuni ya Langchao, ambapo alifahamishwa vilivyo chombo cha huduma cha hali ya juu, Big Data, Mawingu ya mambo ya utawala, na Jukwaa la upashanaji habari katika kituo hiki. Xi Jinping alisema:

  "Hivi sasa tunakaribia zaidi kuliko wakati wowote Ndoto ya China ya kutimiza usitawishaji mkubwa wa Taifa. Safari ya maili 100, hata ukitembea kwa maili 90, ni sawa na kusafiri nusu tu, wakati huu tutakabiliwa na changamoto na taabu kubwa ambazo hazikutokea hapo kabla, wakati huu unatuhitaji tubebe wajibu wa kihistoria, tuungane kwa moyo mmoja, tupige hatua halisi, na kuchapa kazi kutwa kucha. Tunapaswa kujitegemea ili kupata teknolojia muhimu na teknolojia mpya za hali ya juu, ni lazima kukusanya nguvu kwa kufanya jambo kubwa kutokana na nguvu bora ya mfumo wetu."

  Katika Eneo la Sayansi na Teknolojia ya Zhongguancun lililoko pwani ya mji wa Tianjin vimekusanyika viwanda vingi vya teknolojia mpya za hali ya juu. Mwanzoni mwa mwaka huu, Xi Jinping alifanya ukaguzi huko. Meneja mkuu wa Kampuni ya Teknolojia ya udhibiti wa kiakili ya Yifei Bw. Qi Juntong alipomwonesha Rais Xi mfumo wao wa kujidhibiti wa kundi la drone ambao ulivumbuliwa na kampuni hiyo kwa kujitegemea, alimwambia Rais Xi:

  "Hivi sasa sera zilizotolewa na serikali ni kwa ajili ya sisi watafiti na wavumbuzi wa teknolojia tutoe vilivyo nguvu zetu za uhai, tunakuahidi hakika tutatimiza ndoto zetu nyingi."

  Xi Jinping alisema, Chama na Serikali vinajadili kila mara sera za aina mbalimbali kwa ajili ya kujenga mazingira mazuri ya kufanya uvumbuzi.

  "Maendeleo ya sifa bora yanatakiwa kutegemea kazi ya kufanya uvumbuzi, nchi yetu ikitaka kujiendeleza zaidi ni lazima itegemee kazi ya kufanya uvumbuzi kwa kujitegemea. Tunapaswa kuendelea kufanya uvumbuzi, na kuwawezesha watu wenye ndoto ya uvumbuzi wawe na imani thabiti katika kazi ya kufanya uvumbuzi" .

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako