• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda yaanza shughuli mbalimbali za maadhimisho ya wiki ya maombolezo ya mauaji ya kimbari

    (GMT+08:00) 2019-02-09 16:09:15

    Tume ya Taifa ya Rwanda inayopambana na Mauaji ya Kimbari CNLG jana ilizundua shughuli mbalimbali za maadhimisho ya 25 ya mauaji ya kimbari dhidi ya Watusi yaliyotokea mwaka 1994.

    Akiongea na wanahabari mjini Kigali Katibu mtendaji wa CNLG Jean-Damascene Bizimana amesema shughuli hizo zitakazofanyika kwa siku 60 kuanzia Februari 7, zitaangalia zaidi umoja, haki, uwajibikaji, na mapambano dhidi ya itikadi ya mauaji ya kimbari. Shughuli muhimu zitakazofanyika nchi nzima kufuatia maadhimisho ya mwka huu, ni pamoja na vijana kuwatembelea askari wa zamani waliojeruhiwa vitani na kuishi na ulemavu, na wajane waliopoteza watoto wao kwenye mauaji ya kimbari.

    Kwa mwaka huu maadhimisho ya wiki ya maombolezo itaanzia tarehe 1 hadi 13 Aprili ambako hakutakuwepo na burudani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako