• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Xi Jinping anakumbuka maisha ya wananchi   Mambo ya makabila madogo yanayokumbukwa na Xi Jinping

    (GMT+08:00) 2019-02-10 15:47:04

     

    China ni nchi yenye makabila 56, watu wa makabila mengi madogomadogo wanaishi kwenye sehemu zilizoko mbali na pembeni kizazi hadi kizazi. Namna ya kuwafanya watu wa kila kabila dogo waishi kwa furaha katika familia kubwa ya makabila mbalimbali, siku zote ni suala ambalo Rais Xi Jinping analifikiri. Katika kipindi hiki cha "Xi Jinping anakumbuka maisha ya wananchi", leo tunawaletea makala ya sita: Mambo ya makabila madogomadogo yanayokumbukwa na Rais Xi Jinping.

    "Leo ninafuraha sana, nyinyi mmekuja kutoka mbali. Nafurahia hali ya milima kufungwa kwa theluji imeondolewa katika siku za baridi."

    Alisema hayo Rais Xi Jinping alipofanya ukaguzi kwa mara ya kwanza mwaka 2015 kwenye sehemu ya kabila la wadulong mkoani Yunnan. Tarafa ya Dulongjiang iko kwenye Wilaya ya Gongshan mkoani Yunnan, ambayo ni moja kati ya sehemu zilizoko mbali na pembeni zaidi nchini China, hata iliitwa na watu kuwa "sehemu yenye hali duni sana inayowafanya watu waone uchungu kwa sababu ya hali duni ya mawasiliano na huko. Wakati wa mkesha wa Sikukuu ya Mwaka mpya wa 2014, maofisa na watu kadhaa wa sehemu hiyo walimwandikia barua Rais Xi Jinping wakimwambia habari ya kufurahisha, yaani ujenzi wa handaki la barabara ya maskani yao utakamilika, Xi Jinping aliwapongeza. Mwaka mmoja baadaye, Xi Jinping alipofanya ukaguzi mkoani Yunnan, aliwaalika wanakijiji wa kabila la wadulong kwenye hoteli aliyokaa. Alisema:

    "Idadi ya watu wa kabila la wadulong ni zaidi ya watu 6900 tu, lakini wao ni wa familia kubwa ya Taifa la China lenye makabila 56. Sasa sisi sote tuna jukumu takatifu la kutimiza usitawishaji mkubwa wa Taifa, watu wa makabila yote tunatakiwa kubeba jukumu hili, na sehemu zote nchini zinapaswa kujenga jamii yenye maisha bora. Chama na Serikali vitawafuatilia na kuwaunga mkono."

    Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uyghur, eneo lake linachukua moja ya sita ya eneo la China bara, katika eneo hili wanaishi watu wa makabila 47 kama vile wahan, wauyghur, wakhazak na mengineyo, na Rais Xi Jinping anafuatilia sana utulivu na maendeleo ya eneo hilo. Mwezi Aprili mwaka 2014, katika safari yake mkoani Xinjiang alitembelea nyumbani kwa mwanakijiji wa kabila la wauyghur Bw. Abudukeyumo Rouzhi, ambapo aliangalia kwa makini vyumba, jiko, zizi la kondoo, bustani ya matunda na vyombo vya kilimo, na kuwauliza kuhusu hali ya uzalishaji na maisha. Akisema:

    "Safari hii nimefika hapa kuangalia kama sera za Kamati kuu ya Chama zimewanufaisha na kuwafurahisha wananchi. Sera zote za Chama zinapaswa kutungwa na kutekelezwa kwa kulingana na matakwa ya wananchi na kuwanufaisha wananchi."

    Wakati wa mikutano miwili ya Bunge la umma na Baraza la mashauriano ya kisiasa, Rais Xi Jinping aliwahi kuongea na mjumbe wa Bunge la umma kutoka sehemu ya Hetian mkoani Xinjiang Bw. Maitiyibureyimu:

    "Xi Jinping: Najua vijiji vya sehemu ya Hetian vina mashamba machache, katika kijiji chenu kila familia ina hekta ngapi za mashamba?

    Mjumbe: Kila mtu wa familia ana wastani wa hekta 0.08.

    Xi Jinping: Hivi sasa mnapanda nafaka au kupanda miti ya matunda?

    Mjumbe: Miti ya matunda, zaidi ni mikomamanga, halafu tunaweza kupanda baadhi ya nafaka kwenye matuta kati ya miti.

    Xi Jinping: Familia yako inashirikiana na watu wa makabila mengine katika uzalishaji ?

    Mjumbe: Ndiyo tunafanya kazi pamoja na watu kutoka sehemu nyingine katika mabanda ya kupanda mboga, tunaona mshikamano wa makabila mbalimbali ni muhimu.

    Xi Jinping: Ni lazima kufanya mashikamano wa watu wa makabila mbalimbali, mmefanya mambo muhimu sana."

    Mwezi Juni mwaka 2016, Rais Xi Jinping alifanya ukaguzi mkoani

    Ningxia alikumbuka akisema:

    "Nilipofika sehemu ya Haigu ya mkoa huo, nilishtushwa na hali mbaya ya umaskini ya sehemu hiyo, nilidhamiria kutekeleza mpango na maamuzi ya Kamati kuu ya Chama, kuhimiza Mkoa wa Fujian na Mkoa wa Ningxia isaidiane, na kuwasaidia watu walioishi kwenye sehemu yenye hali duni wahamie kwenye sehemu zinazofaa kuzalisha mazao na kuishi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako