• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Xi Jinping anakumbuka maisha ya wananchi---Kwanini Katibu Mkuu wa Chama anampongeza Ndugu Ma?

  (GMT+08:00) 2019-02-11 07:37:54

  Mwaka 2018 Kamati Kuu ya Chama na Baraza la serikali la China vilitoa tuzo kwa watu mia moja waliotoa mchango mkubwa katika mambo ya mageuzi na ufunguaji mlango, na Bw Ma Shanxiang alisifiwa kuwa mtangulizi wa mageuzi. Katika kipindi hiki cha "Xi Jinping anakumbuka maisha ya wananchi", leo tunawaletea makala ya saba kuhusu Ndugu Ma aliyepongezwa na Katibu mkuu wa Chama. 

  "Mimi ni Ma Shanxiang, ni mkuu wa "Ofisi ya kazi ya Mzee Ma" kwenye Mtaa wa Guanyinqiao mjini Chongqing, nimefanya kazi ya usuluhishi wa migongano kati ya wakazi kwa miaka 30, ambapo nimeandika kumbukumbu za kazi kwenye madaftari zaidi ya 160, na kufanya majumuisho ya mbinu za aina zaidi ya 60 za kusuluhisha migongano…"

  Bw. Ma alikuwa msuluhishi kwenye ofisi ya mtaa baada ya kumaliza muda wake jeshini mwaka 1988. Katika miaka 30 iliyopita, anawasaidia wakazi wa huko kutatua matatizo, na kusuluhisha matukio zaidi ya elfu mbili ya migongano kati ya watu. Mpaka sasa ameshastaafu lakini bado anatoa mchango kwenye "Ofisi ya kazi ya Mzee Ma". Alisema:"Kwenye jamii ya mashinani, mara kwa mara tunaweza kukutana na migongano kati ya wakazi, au malalamiko ya watu juu ya kuhamia, juu ya wasimamizi wa mji, migongano kati ya wakazi na wasimamizi wa eneo la makazi, ama migongano kwenye familia kuhusu mali, wasuluhishi wanatakiwa kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kufanya kazi.

  Nnakumbuka niliposuluhisha migongano kati ya wajenzi wa barabara na maduka 22 kando ya barabara, tukio hili lilihusisha watu zaidi ya mia moja, lakini tuliwabembeleza watu kwa uvumilivu na kushughulikia kwa makini hali tofauti, mwishowe tulitatua vizuri mgongano huu. Kweli tunatakiwa kushughulikia masuala kuhusu kujiendeleza, huku tukishughulikia matatizo ya kuwafanya watu wawe na masikilizano."

  Hivi sasa "Njia za kufanya usuluhishi za Mzee Ma" zimekuwa vielelezo kwa wanaofanya kazi mashinani katika sehemu mbalimbali nchini China. Na akipata nafasi, Bw. Ma anakwenda mitaani na kwenye maeneo ya makazi mbalimbali kuwasaidia watu kupata uzoefu wa kushughulikia kazi. Alisema: 

  "Ofisa mmoja akiwa na hisia za upendo kwa Chama, akiwa na nia na imani thabiti, na awe na uwezo wa kuwatumikia watu kwa uchangamfu, hakika atakaribishwa na watu popote anapokwenda."

  Baada ya kusikiliza hotuba ya Bw. Ma, Katibu Mkuu wa Chama alisema, Jengo Kuu la Ujamaa wenye umaalumu wa China linapaswa kutegemea mihimili na nguzo mbalimbali, uongozi wa Chama ni msingi, na Kamati Kuu ya Chama ni Uti wa mgongo, vilevile linahitaji msingi imara wa mashinani. Akisema:

  "Ni lazima tuimarishe msingi mashinani. Kama msingi huo hautakuwa wa imara, ardhi itatetemeka, na milima itatikisika. Tunahitaji mamia na maelfu ya maofisa wa mashinani kama Mzee Ma, ili wafanye kazi ya utangulizi wa wanachama, natumai Mzee Ma ataendelea kufanya vizuri kazi mbalimbali, na kupata mafanikio kwa mara nyingine tena".

  Wakati wa mikutano miwili ya taifa, Bw. Ma aliandika kumbukumbu nyingi kuhusu misingi ya mikutano hiyo, alisema atawaambia watu wengine yote hayo, na yeye mwenyewe ametiwa moyo sana na Katibu mkuu wa Chama, ataendelea na juhudi za kuwatumikia watu wa mashinani na kuitumikia jamii. Akisema:

  "Katibu Mkuu Xi wa Chama alipopeana mkono na mimi alinisifu kwa kutoa ripoti nzuri, naona fahari kubwa, nitabeba wajibu wangu nikiwa mwanachama wa mashinani, nitafanya kazi yangu ya kuwawezesha watu waone matumaini katika uzalishaji na maisha."

  Maelezo kuhusu Katibu mkuu kupongeza Mzee Ma inaishia hapa, lakini Mzee Ma na wengine wengi mashinani wanaendelea kuchapa kazi kufuata maagizo aliyotoa Katibu mkuu wa Chama Xi Jinping.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako