• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika watarajia kuzindua operesheni za Eneo la biashara huria la Bara la Afrika mwezi Julai

    (GMT+08:00) 2019-02-11 09:27:19

    Kamishna wa biashara na viwanda wa Umoja wa Afrika Bw. Albert Muchanga amesema anatarajia kuwa Eneo la Biashara huria la Bara la Afrika AfCFTA litazinduliwa rasmi mwezi Julai mwaka huu.

    Akiongea na wanahabari kando ya mkutano wa 32 wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Bw. Muchanga amesema kuanzishwa rasmi kwa operesheni za Eneo la biashara huria la Afrika kunatarajiwa kuzinduliwa kwenye mkutano mwingine wa kilele wa Umoja wa Afrika utakaofanyika mjini Niamey, Niger mwezi Julai.

    Kamishna huyo amesema baada ya eneo hilo kuanza kazi mwezi Julai, Umoja wa Afrika unatarajia kuwa nchi wanachama wake wataanza kuboresha mahusiano ya kibiashara kati yao, kupunguza ushuru wa forodha kati ya nchi za Afrika na kuwa na utaratibu wa kusimamia matumizi ya vizuizi visivyo vya ushuru.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako