• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwenyekiti wa SADC afanya mazungumzo na mkuu wa UM juu ya hali ya Zimbabwe na DRC

    (GMT+08:00) 2019-02-11 09:27:40

    Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC na rais wa Namibia Bw. Hage Geingob amefanya mazungumzo na katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw. Antonio Guterres kuhusu machafuko ya kisiasa nchini Zimbabwe na Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC.

    Taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais wa Namibia imesema rais Geingob alikutana na katibu mkuu wa Umoja wa mataifa kando ya mkutano wa Umoja wa Afrika unaoendelea nchini Ethiopia, kwa ajili ya kumpa mrejesho juu ya hali ya sasa nchini Zimbabwe na DRC.

    Imefahamika kuwa Zimbabwe inashuhudia mgogoro wa kiraia kutokana na gharama kubwa za maisha, huku DRC ikiwa kwenye msukosuko wa kisiasa tangu Bw. Felix Tshisekedi achaguliwe kuwa rais mpya wa nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako