• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kilele wa AU wajadili suala la wakimbizi na usalama barani Afrika

    (GMT+08:00) 2019-02-11 09:34:10

    Mkutano wa kilele wa 32 wa Umoja wa Afrika unaendelea kufanyika huko Addis Ababa, na kujadili masuala makuu yanayolikabili bara hilo, likiwemo suala la wakimbizi, amani na usalama.

    Mkutano huo wa siku mbili wenye kaulimbiu ya "Wakimbizi, Waliorejea nyumbani na Wakimbizi wa ndani: kutafuta utatuzi wa kudumu kwa wakimbizi barani Afrika", utajadili masuala kuhusu mageuzi ya idara za Umoja wa Afrika, eneo la biashara huria la Afrika miongoni mwa miradi na mapendekezo ya bara hilo.

    Mwenyekiti wa kamati ya Umoja huo Bw. Moussa Faki Mahamat amesema, suala la wakimbizi barani humo bado ni la kuhuzunisha, na kwamba ni muhimu kutatua kwa kina chanzo kikuu cha hali hiyo wakati operesheni za shirika la kibinadamu la Afrika zikiendelea kuharakishwa.

    Bw. Mahamat pia amepongeza maendeleo katika mchakato wa amani na makubaliano katika kanda ya Afrika, hata hivyo ameeleza wasiwasi wake juu ya hali iliyopo huko Sahel na maeneo ya ziwa Chad, huku akihimiza kuimarisha mshikamano katika kushughulikia suala hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako