• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wageni watoa maoni yao kuhusu mwaka mpya wa jadi wa China

    (GMT+08:00) 2019-02-11 19:08:17

    Katika miaka ya hivi karibuni, kadiri mchakato wa mageuzi na ufunguaji mlango unavyopiga hatua kwa haraka zaidi, ndivyo wageni wengi wanavyozidi kufahamu, kuelewa na kupenda utamaduni wa Mwaka mpya wa jadi wa China yaani Sikukuu ya Spring ambayo inamaanisha matumaini makubwa, upendo, masikilizano na kukutana kwa familia yote. Sikukuu ya Spring ya China imekuwa dirisha muhimu kwa dunia kuelewa utamaduni wa China.

    Wakati wa Sikukuu ya Spring, sehemu nyingi zenye vivutio vya utalii mjini Beijing kama vile Kasri la Kifalme, na Njia ya Nanluogu, zinawavutia watalii wengi ambao wanafahamu na kujiburudisha sikukuu hiyo yenye neema kubwa.

    "Sikukuu ya Sping ni muhimu sana, kwani watu wanaagana na mwaka uliopita huku wakikaribisha mwaka mpya kwa kulipua fataki, na watu wanasherehekea sikukuu hiyo kubwa pamoja na familia yote."

    Mbali na Beijing, shughuli mbalimbali za jadi za China kama vile Miaohui yaani Magulio ya Hekalu, kupiga kitendawili, na kucheza ngoma ya dragoni vilevile zinafanyika katika sehemu mbalimbali. Jelica Cpic kutoka Serbia anasema, Sikukuu ya Spring ya China inafanana na sikukuu ya nchi za magharibi, kwani watu wote wa familia husherehekea sikukuu hiyo kwa kula pamoja. Anasema:

    "Sikukuu ya Spring inamaanisha kuwa watu wa familia moja wanakula vyakula vingi kwa pamoja. Hususan wanakula Jiaozi na mtu atakayekula Jiaozi inayotofautiana na nyingine atapata fedha nyingi zaidi na neema kubwa zaidi katika mwaka mpya."

    Mbali na shughuli mbalibali, kwenda kutalii vilevile ni tabia mpya ya wachina katika kusherehekea Sikukuu ya Spring. Kwa mujibu wa takwimu za Taasisi ya utafiti wa utalii ya China, wakati wa Sikukuu ya Spring ya Mwaka 2019, idadi ya watalii nchini China imefikia milioni 415, likiwa ni ongezeko la asilimia 7.6, pato la utalii ni RMB yuan bilioni 513.9, sawa na dola za kimarekani bilioni 76.7, likiwa ni ongezeko la asilimia 8.2. Rhio kutoka Ufilipino ambaye alikwenda mji wa Chengdu kusherehekea sikukuu hiyo pamoja na familia yake anasema:

    "Sikukuu ya Spring ni muhimu kwa China na kila mtu wa China, ambayo inamaanisha watu kutumiana salamu za heri, pia inaleta matumaini makubwa kwa kila mtu."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako