• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Moto Hauzimwi uwanja wa Taifa, Leo ndio Leo- Simba vs Al Ahly

  (GMT+08:00) 2019-02-12 08:12:02
  Wapenda soka wanasema mtoto hatumwi dukani, leo katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam kutatimuka vumbi kwa Simba ya Tanzania itakapomenyana na Al Ahly ya Misri katika mchezo wa marudiano wa kundi D michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

  Katika mchezo wa kwanza uliofanyika wiki iliyopita jijini Alexandria Misri, Al Ahly iliifunga Simba goli 5-0.

  Kuelekea mchezo huo, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Simba SC ambaye pia ni muwekezaji wa klabu hiyo Mohammed Dewji amewataka watanzania na wana Simba waiunge mkono timu yao kwani, wanatakiwa kufahamu kuwa Simba imekutana na timu zenye nguvu zaidi yao lakini hiyo haiwakatishi tamaa ya kusema kuwa timu yao haiwezi kufanya chochote katika michuano hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako