• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Sangoma wa Man U kiboko, Cavani aumia, Mbappe apewa jukumu zito

  (GMT+08:00) 2019-02-12 08:13:40

  Kama Manchester United inatumia mganga kuelekea mechi yake ya leo ya hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Paris Saint Germain basi inabidi imlipe dau la kutosha. Baada ya uhakika wa kumkosa Neymar aliyepata jeraha la kifundo cha mguu, PSG leo pia itamkosa Edinson Cavani ambaye ameumia mwishoni mwa wiki kwenye mtanange dhid ya Bordeaux.

  Kocha wa PSG, Thomas Tuchel atalazimika kumpanga mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Kylian Mbappe kama mshambuliaji wa kati huku kushoto akicheza Julian Draxler na kulia akikaa Angel Di Maria.

  Pambano la marudiano baina ya Machester United na PSG linatazamiwa kupigwa Machi 3 katika uwanja wa Old Trafford jijini Manchester na kuna uwezekano Cavani akarudi katika mechi hiyo lakini hakuna uwezekano wa Neymar kucheza mechi hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako