• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • UM yatoa wito wa kuchukua hatua kuhakikisha usalama wa walinzi wa amani

  (GMT+08:00) 2019-02-12 09:51:39

  Wajumbe kadhaa wa Umoja wa Mataifa wametoa wito wa kuhakikisha usalama wa walinzi wa amani.

  Ripoti ya katibu mkuu wa umoja huo iliyotolewa kwenye mkutano wa 258 wa kamati ya operesheni za kulinda amani ya umoja huo, imesisitiza maendeleo muhimu na kusema kubadilika kwa vyanzo vya migogoro kumeongeza hatari kubwa ya usalama dhidi ya walinzi hao. Pia imesema, idadi ya vifo vya walinzi hao imeongezeka karibu maradufu katika mwaka 2017, kutoka 34 ya mwaka 2016 hadi 61. Ripoti pia imesema gharama za jumla katika kuhakikisha usalama na operesheni kamili zimefikia dola za Marekani milioni 250 kwa mwaka.

  Naibu balozi wa China katika umoja huo Bw. Wu Haitao amesema, umoja huo unapaswa kuboresha mfumo wa misaada, kuimarisha mafunzo ya walinzi na kuongeza uwezo wao wa kukabiliana na hali ngumu ili kuongeza usalama wa walinzi wa amani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako