• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mji wa Shanghai kuimarisha mageuzi na ufunguaji mlango

    (GMT+08:00) 2019-02-12 10:27:55

    Rais Xi Jinping wa China aliwahi kushiriki kwenye majadiliano ya ujumbe wa Shanghai kwenye mikutano ya mwaka ya bunge la umma la China na Baraza la mashauriano ya kisiasa la China kwa miaka mitano mfululizo, amezungumzia mageuzi, uvumbuzi na utawala, kudhihirisha mawazo na njia ya maendeleo, na kuwapa moyo wakazi wa Shanghai. Picha zifuatazo zinaonesha jinsi mji wa Shanghai ulivyotekeleza maneno muhimu ya rais Xi, kuimarisha imani na nia ya kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, na kuhudumia kazi ya jumla ya mageuzi na ufunguaji mlango nchini China.

    1. Rais Xi Jinping akishiriki kwenye majadiliano ya ujumbe wa Shanghai kwenye mkutano wa mwaka 2017 wa bunge la umma la China, na kusema China haitaacha sera ya ufunguaji mlango, itaendelea kufungua mlango katika pande zote, na kusukuma mbele biashara na uwekezaji huria na kurahisisha mambo hayo.

    2. Mwezi uliopita, kiwanda cha kwanza cha kampuni ya Tesla kilichoko nje ya Marekani kilizinduliwa mjini Shanghai. Mkurugenzi mtendaji mkuu wa kampuni hiyo Bw. Elon Musk alisema kiwanda hiki kisingepata maendeleo hayo makubwa bila ya uungaji mkono wa serikali ya Shanghai, kiwanda hiki hakika kitakuwa kimoja cha viwanda vizuri zaidi duniani.

    3. Naibu mkurugenzi wa kamati ya usimamizi wa eneo la Lingang Bw. Chenjie alisema eneo hili linashikilia kazi ya ufunguaji mlango, ambayo ni matakwa ya rais Xi Jinping kuhusu uchumi wa China.

    4. Mkurugenzi mtendaji mkuu wa kampuni ya ABB Bw. Ulrich Spiesshofer alisema kampuni yake imepata fursa ya kuanzisha shughuli ya mashine zinazojiendesha na akili bandia mjini Shanghai, na hakika mji huo utatangulia katika shughuli ya utengenezaji wa mashine zinazojiendesha duniani.

    5. Katibu wa kamati ya chama wa kampuni ya Huahong ya Shanghai Bw. Zhang Suxin alisema kampuni yake itaendelea kuongeza nguvu kufanya uvumbuzi, ili kuinua teknolojia na uwezo wa utafiti na usanifu.

    6. Naibu katibu mkuu wa serikali ya Shanghai ambaye pia ni mkurugenzi wa kamati ya maendeleo na mageuzi Bw. Ma Chunlei alisema wakazi wa Shanghai watakumbuka maneno muhimu ya rais Xi Jinping, na kusukuma mbele maendeleo ya mji huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako