• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mustakabali mzuri wa soko la China wavutia uwekezaji kutoka nchi za nje

  (GMT+08:00) 2019-02-12 17:19:11

  Wizara ya Biashara ya China imetangaza kuwa, mwaka 2018 China imejenga kampuni 60,533 zinazowekezwa na wafanyabiashara nchini China, likiwa ni ongezeko la asilimia 69.8; matumizi ya fedha yamefikia dola za kimarekani bilioni 130.2, likiwa ni ongezeko la asilimia 0.9. Mwaka jana wakati dunia nzima ilipokabiliwa na changamoto za kuvutia fedha za kigeni, China ilipata ongezeko kubwa katika sekta hiyo, hali ambayo imeonesha mustakabali mzuri wa soko la China.

  Mwaka jana matumizi ya fedha za kigeni ya China yameonesha umaalumu wa kipekee katika pande tatu zikiwa ni pamoja na: muundo wa uwekezaji wa kigeni umeboreshwa. Takwimu zimeonesha matumizi ya fedha za kigeni katika viwanda vya utengenezaji nchini China yameongezeka hadi asilimia 30.6, huku yakiongezeka kwa asilimia 35.1 katika viwanda vya utengenezaji wa teknolojia ya hali ya juu.

  Uwekezaji katika sehemu ya magharibi na ya kati nchini China umeongezeka kwa kasi. Mwaka jana sehemu za magharibi zimetumia dola za kimarekani 9.5, likiwa ni ongezeko la asilimia 18.5; matumizi ya fedha za kigeni katika sehemu za kati yamefikia dola za kimarekani bilioni 9.53, ikiwa ni ongezeko la asilimia 15.4.

  Uwekezaji kutoka kundi la kiuchumi lililoendelea duniani. Mwaka 2018 uwekezaji kutoka Uingereza, Ujerumani, Korea ya Kusini, Japan na Marekani nchini China umeongezeka kwa asilimia 150.1, 79.3, 24.1, 13.6 na 7.7.

  Wakati mazingira ya uwekezaji duniani yanapozorota kutokana na kujilinda kibiashara, utaratibu wa upande mmoja na siasa inayojali maoni na fikra za umma, uwekezaji ukizidi kuvutiwa nchini China kutokana na mustakabali mkubwa wa soko la China, na nia thabiti ya China katika kufungua mlango na kuzidi kuboresha mazingira ya uendeshaji wa biashara. Tangu mwaka jana China imetekeleza hatua mbalimbali za kuvutia uwekezaji. Afisa mtendaji mkuu wa kampuni ya Tesla Bw. Elon Musk anaona kuwa, sera ya mageuzi na ufunguaji mlango ya China imetekelezwa kwa hatua halisi. Meneja mkuu wa kampuni ya IKEA Bibi Anna Pawlak-Kuliga pia ameeleza kuwa, juhudi za serikali ya China katika kuboresha mazingira ya uendeshaji wa biashara zimewaachia watu picha kubwa.

  Tukitupia macho dunia nzima, ni vigumu kupatikana soko kama la China ambalo lina mustakabali mzuri wa matumizi ya fedha huku likiandaa mazingira mazuri kwa maendeleo ya uwekezaji wa kigeni. Kama ilivyopanga, China itaendelea kutekeleza hatua mbalimbali ili kuviwezesha viwanda vinavyowekezwa kwa fedha za kigeni kunufaika zaidi na kupata maendeleo makubwa zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako