Simba sasa imefufua matumaini ya kwenda robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya ushindi wa goli 1-0 dhidi ya timu bora Afrika Al Ahly ya Misri katika mchezo wa kundi D uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Alikuwa mchezaji raia wa Rwanda anayechezea klabu hiyo ya Simba Meddy Kagere ndiye aliyewanyanyua mashabiki waliofurika kushuhudia Muarabu akipigishwa kwata.
Katika mchezo mwingine wa kundi hilo, JS Saoura ya Algeria imeitwanga AS Vita ya DRC kwa bao 1-0. Kwa ushindi huo, Saoura iliyokuwa nyumbani Algeria, unafanya Simba kubaki katika nafasi ya pili, Al Ahly wakiongoza kundi hilo, huku Saoura na Vita wakiwa katika nafasi ya tatu na ya nne.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |