• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yawawekea karantini watu 13 waliogusa mwili wa mtu anayehisiwa kufariki kwa Ebola

    (GMT+08:00) 2019-02-13 09:43:37

    Mamlaka nchini Uganda zimewawekea karantini watu 13 waliosafirisha mwili wa mtu anayehisiwa kufariki kwa homa ya Ebola kutoka mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC.

    Wizara ya afya ya Uganda na Shirika la afya duniani WHO limesema kupitia taarifa kuwa, jamaa 13 wa marehemu huyo mwenye umri wa miaka 46 walikwenda kwenye hospitali ya Bunia nchini DRC kurudisha mwili wake kwa ajili ya mazishi kwenye eneo la mashariki la Tororo nchini Uganda.

    Taarifa hiyo ya pamoja inasema marehemu huyo alipatiwa matibabu kwenye hospitali ya Bunia kuanzia mwezi Novemba mwaka jana kutokana na maumivu ya kifuani na kukohoa damu, na alifariki dunia Ijumaa baada ya hali yake kuwa mbaya wiki iliyopita.

    Taarifa pia imesema mpaka sasa hakuna maambukizi ya homa ya Ebola yaliyoripotiwa nchini Uganda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako