• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM yaunga mkono ushiriki wa wanawake kwenye ujenzi wa amani kwenye eneo la maziwa makuu Afrika

    (GMT+08:00) 2019-02-14 08:51:11

    Ofisa wa Umoja wa mataifa amesema jumuiya ya kimataifa itaunga mkono ushiriki wa wanawake kwenye programu zinazolenga kuhimiza suluhu ya migogoro katika eneo la Maziwa makuu barani Afrika.

    Mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa kwa eneo la Maziwa makuu Bw. Said Djinnit, amesema ushiriki mkubwa wa wanawake ni muhimu katika kutimiza amani ya kudumu, usalama na maendeleo ya kiuchumi kwenye eneo hilo ambalo limeshuhudia migogoro ya kiraia kwa muda mrefu.

    Akiongea mjini Nairobi kwenye mkutano wa kujadili mfumo wa UM unaolenga kuimarisha ushiriki wa wanawake katika utatuzi wa migogoro kwenye eneo la Maziwa makuu, Bw. Djinnit amezihimiza serikali kuharakisha utekelezaji wa asilimia 30 ya uwakilishi wa wanawake kwenye vyombo vya kisiasa na kujenga amani, kama ilivyokubaliwa na nchi za maziwa makuu mwezi Novemba mwaka jana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako