• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • WFP inatarajia kuwa pande zinazopambana Yemen zitafikia makubaliano

    (GMT+08:00) 2019-02-15 09:17:42

    Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP linatarajia kuwa pande zinazopambana nchini Yemen zitafikia makubaliano ya kufanikisha wafanyakazi wa misaada wa Umoja wa mataifa, kufika kwenye bandari ya Hodeidah kwenye maghala ya chakula ya WFP.

    Mwakilishi wa WFP nchini Yemen Bw. Stephen Anderson amesema eneo hilo la bandari lina utatanishi sana kwa kuwa liko kwenye mstari wa mbele wa mapambano na sio rahisi kulifikia.

    Msemaji wa Umoja wa mataifa Bw. Stephen Dujarric amesema karibu watu milioni 24 nchini Yemen, ambao ni asilimia 80 ya watu wote, wanahitaji msaada wa kibinadamu na ulinzi nchini Yemen, na kufanya msukosuko wa nchi hiyo kuwa mbaya zaidi duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako