• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • RIADHA: IAAF yakana kuwatambua kama wanaume wanariadha wote wanawake wenye homoni nyingi za kiume

  (GMT+08:00) 2019-02-15 09:23:06

  Shirikisho la riadha duniani IAAF limekana kwamba litaiambia mahakama kuwa wanariadha wote wanawake wenye homoni nyingi za kiume mwilini, kama vile Caster Semenya wanapaswa kutambuliwa kama wanaume. Bingwa wa dunia na Olimpiki katika mbio za mita 800 anapinga sheria iliyopendekezwa na IAAF inayonuiwa kudhibiti viwango vya homoni hiyo kwa wanariadha wanawake. Kesi hiyo itasikilizwa katika mahakama ya malalamiko katika michezo (Cas) wiki ijayo. Gazeti la the Times limeripoti kuwa mawakili wa IAAF watasema kuwa Semenya "kibaolojia ni mwanamume" pamoja na kwamba anatambuliwa kuwa mwanamke. Shirikisho hilo la riadha linasema "halitambui" mwanariadha yoyote mwenye "tofuati za kukuwa kijinsia" (DSD) - ambapo Semenya ndiye anayeonekana zaidi - kuwa mwanamume. IAAF ilinuia kuidhinisha sheria mpya Novemba 1 mwaka jana lakini ikaahirisha hadi Machi 26 kusubiri matokeo ya kesi aliyowasilisha Semenya na shirikisho la riadha Afrika kusini. Kuahirishwa huko kunamaanisha kuwa wanariadha wenye hali hiyo ya DSD hawataruhusiwa kushiriki mashindano kwa miezi 6 kutoka tarehe ambayo mabadiliko ya sheria yataidhinishwa ambayo huenda ikamfanya Semenya akase kushiriki baadhi ya mashindano ya msimu wa 2019.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako