• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China akutana na mjumbe wa biashara wa Marekani

  (GMT+08:00) 2019-02-15 21:53:37

  Rais Xi Jinping wa China amekutana na mjumbe wa biashara wa Marekani Bw. Robert Lighthizer na waziri wa fedha Bw. Steven Mnuchin ambao wako hapa Beijing kushiriki kwenye duru ya sita ya majadiliano ya ngazi ya juu kuhusu uchumi na biashara kati ya nchi hizo.

  Rais Xi amezitaka pande hizo mbili kufuata kanuni na mwelekeo uliowekwa alipokutana na rais Donald Trump wa Marekani nchini Argentina, na kuimarisha mawasiliano, kufuatilia ushirikiano, kudhibiti migongano, ili kusukuma mbele ushirikiano wa uchumi na bishara kati ya nchi hizo mbili na maendeleo ya uhusiano kati ya nchi mbili.

  Hatua hiyo imeonesha mazungumzo hayo yamepata maendeleo makubwa baada ya yale yaliyofanyika wiki mbili zilizopita mjini Washington. Wachambuzi wanaona kuwa, China ina nia ya dhati katika kutatua suala la uchumi na biashara kati ya pande hizo mbili kwa njia ya ushirikiano. Wanaona kuwa pande hizo mbili zimefanya mazungumzo kwa kina na kufikia makubaliano katika masuala muhimu ambayo yanazingatia ufuatiliaji wa pande zote mbili, na kuzingatia kanuni za usawa na kunufaishana.

  Mbali na hayo China na Marekani zimejadili makubaliano kuhusu masuala ya uchumi na biashara, ambayo imeonesha mazungumzo hayo yameingia katika kipindi cha kuandaa makubaliano, ambacho ni maendeleo muhimu. Tena pande hizo zitafanya mawasiliano zaidi kuhusu utaratibu wa utekelezaji, hatua itakayosaidia kuhakikisha kithabiti utekelezaji wa hatua zilizoamuliwa kwa pamoja na pande zote mbili.

  Linalofuatiliwa zaidi ni kwamba, ujumbe wa uchumi na biashara kati ya China na Marekani umeamua kuendelea na mazungumzo wiki ijayo mjini Washington, hatua ambayo imeonesha pande zote mbili zina matumaini makubwa ya kufikia makubaliano ndani ya muda uliowekwa.

  Roma haikujengwa kwa siku moja, ndivyo migogoro ya uchumi na biashara kati ya makundi hayo makubwa ya kiuchumi haitafumbuliwa kabisa ndani ya siku 90. Bado inapaswa kuchukua msimamo wa tahadhari juu ya matokeo ya mwisho, lakini watu wanachukua msimamo chanya juu ya kufikiwa kwa makubaliano ya uchumi ambayo yananufaisha pande zote mbili.

  Endapo pande hizo mbili zitaendelea kufanya juhudi za kusaidia, uhusiano kati yao utashinda migogoro na kupata matokeo ya kunufaishana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako