• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Hatua kubwa yapigwa mbele katika mjadala wa China na Marekani

  (GMT+08:00) 2019-02-16 09:04:58
  Mjadala wa 6 wa ngazi ya juu kuhusu mambo ya kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani ulimalizika jana hapa Beijing. Kwa mara ya kwanza rais Xi Jinping wa China alikutana na ujumbe wa Marekani tangu hali ya mvutano ianze kupanda ngazi mwezi Februari mwaka jana.

  Kwenye mkutano huo, rais Xi alitaja kwa mara kadhaa neno la "ushirikiano" , akisema siku zote China ina matumaini kwamba, mgogoro huo ungetatuliwa kwa njia ya ushirikiano. Vile vile alisisitiza kuwa, ushirikiano huo una msingi wake kwamba, China haikubali maslahi yake kuu iharibiwe.

  Katika duru hiyo ya mjadala uliofanyika hapa Beijing, pande mbili zilibadilishana maoni kwa kina kuhusu mambo mbalimbali, kama vile kutoa tekenolojia, kulinda halimiliki ya ujuzi, vikwazo vya biashara visivyo vya ushuru wa forodha, sekta ya huduma, sera ya kilimo, uwiano wa biashara na hatua za kutekeleza makubaliano yatakayofikiwa. Inaonekana kwamba, maoni ya pamoja yanaongezeka huku tofauti kupungua.

  Pande hizo mbili pia zilijadiliana nakala ya makubaliano ya mwanzo, jambo ambalo linaonyesha kuwa, mjadala huo umepiga hatua muhimu mbele kwa kufikia kipindi cha utungaji wa nakala ambayo itaweza kuwa msingi wa makubaliano ya mwisho. Pande zote mbili zilikubaliana kuendelea na mjadala huo wiki ijayo huko Washington, ambayo ni ishara kwamba zinapenda makubaliano yangefikishwa kabla ya tarehe 1Machi.

  Maendeleo hayo si kama tu yanalingana na maslahi ya China na Marekani, bali pia nchi nyingine duniani, ambapo masoko muhimu ya hisa yalipanda juu mara baada ya mjadala huo kumalizika, hali ambayo inaonyesha kuwa watu wanapenda kuona nchi hizo mbili zingefikia makubaliano.

  Hata hivyo matatizo yanayochanganyika ya kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani ambazo zina uchumi mkubwa zaidi duniani, hayatatatuliwa kabisa ndani ya miezi kadhaa tu. Katika miaka 40 iliyopita tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kibalozi, misukosuko ilitokea mara kadhaa, lakini yote iliondolewa kutokana na busara za viongozi wa nchi mbili. Habari zilizotolewa kutoka kwa upande wa Marekani zinasema, marais wa nchi mbili watakutana kwa mara nyingine tena hivi karibuni. Watu wana sababu ya kuwa na imani kwamba, pande hizo mbili zitafikia makubaliano ambayo ni ya haki na kila upande unanufaika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako