• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Makubaliano ya biashara kati ya China na Marekani kunufaisha uchumi wa dunia

  (GMT+08:00) 2019-02-18 16:27:35

  Duru ya sita ya mazungumzo ya ngazi ya juu kuhusu mambo ya kibiashara kati ya China na Marekani imefungwa mjini Beijing. Pande hizo mbili zimeafikiana kuhusu masuala muhimu. Wataalamu wanaona China na Marekani zikifikia makubaliano kuhusu biashara, uchumi wa dunia utanufaika.

  Ili kutekeleza maoni ya pamoja ya viongozi wa China na Marekani yaliyofikiwa kwenye mkutano wa Argentina, kuanzia tarehe 14 hadi 15, nchi hizo mbili zimefanya mazungumzo kwa kina kuhusu masuala yanayofuatiliwa na pande hizo mbili ikiwemo mauzo ya teknolojia, ulinzi wa haki miliki za kiubunifu, vikwazo vya kibiashara, sekta za huduma na kilimo, uwiano wa biashara, na mfumo wa utekelezaji. Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa mambo ya fedha ya taifa ya Chuo Kikuu cha Qinghua Bw. Zhu Min, aliyekuwa naibu mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF anaona kuwa mazungumzo ni mwanzo mzuri wa utatuzi wa mvutano wa kibiashara kati ya China na Marekani. Anasema,

  "Mazungumzo hayo yametaja mambo mengi, tumeafikiana kuhusu masuala mengi, lakini bado tuna maoni tofauti. Biashara huleta mazungumzo, na mazungumzo ni mwanzo mzuri. Hivi sasa Marekani pia inaona mazungumzo ni njia mwafaka ya kutatua masuala."

  Duru hii ya mazungumzo ni muhimu zaidi katika mwaka uliopita, na imetiliwa maanani na pande hizo mbili. Mwenyekiti wa Shirikisho la Wafanyabiashara wa Marekani nchini China Bw. Xia Zunen anasema,

  "China na Marekani zinaelewa kanuni za biashara kwa njia tofauti, na hali hii imeleta matatizo mengi. Inatubidi kutafuta utatuzi wa suala hilo, au tufafanue zaidi kanuni hizo, au tufanye marekebisho. Tukiweza kutatua suala hilo, na kuondoa athari iliyosababishwa na tatizo hilo kwa biashara kati ya nchi hizo mbili, uchumi wa dunia nzima pia utanufaika."

  Baada ya duru hiyo, China na Marekani pia zinatarajiwa kufanya duru nyingine ya mazungumzo mjini Washington, Marekani wiki ijayo. Katibu mkuu wa Mfuko wa Utafiti wa Maendeleo ya China Bw. Lu Mai ana matumaini kuhusu mustakabali. Anasema,

  "Watu wote wanatumai kupunguza hali ya utatanishi, lakini inachukua muda kufikia makubaliano ya mwisho. Bado safari ni ndefu. China inafuata njia yake, ambayo ni endelevu na italeta mustakabali mzuri."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako