• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Vyama vya ushirika vyasitisha shughuli mtwara kuhusu malipo ya korosho

    (GMT+08:00) 2019-02-18 20:16:23

    Vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) mkoani Mtwara, vimesitisha shughuli za ushirika kwa madai ya kucheleweshwa kulipwa fedha za ushuru Sh. 70 kwa kila kilo moja ya korosho, ambazo hutumika kuendesha shughuli za vyama hivyo katika msimu huu 2018/2019.

    Wakizungumza na waandishi wa habari mjini Mtwara, viongozi wa vyama hivyo kutoka wilaya tano, walisema malipo ya shilingi 70 kwa kilo moja ya korosho yako kisheria, hivyo kukosa malipo hayo mapema, vyama vimeshindwa kujiendesha.

    Hata hivyo serikali mwezi huu imeanza kuingiza fedha hizo kwenye vyama vya msingi kwa kuanza na Sh. 14,000 kwa ajili ya kuwalipa makarani waliokuwa wanapokea korosho na wachukuzi waliokuwa wakipakia magunia ya korosho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako