• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga lawama za Marekani kuhusu Huawei

    (GMT+08:00) 2019-02-19 14:12:55

    Wizara ya mambo ya nje ya China imepinga lawama za Marekani kuhusu Huawei, na kuzitaka nchi zote zifuate kanuni ya ushindani wa haki na kulinda kwa pamoja mazingira ya haki na yasiyo ya ubaguzi.

    Habari zimesema kwenye mkutano wa usalama uliofanyika Jumamosi iliyopita huko Munich, makamu wa rais wa Marekani Bw. Mike Pence alionya kuwa washirika wa Marekani wanakabiliawa na "tishio" la kampuni ya Huawei ya China wakati inapotafuta washirika kujenga miundo mbinu ya wireless ya 5G. Baadhi ya maofisa wa Marekani hivi karibuni walisema, kutokana na Sheria ya Intelijinsia ya China, kampuni zikiwemo Huawei na ZTE zinaweza kulazimishwa kutoa data kwa idara za ujasusi za China.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari, kuwa huu ni uelewa mbaya kuhusu sheria husika za China.

    Bw. Geng amesema, Sheria ya Intelijinsia ya China si kama tu inasisitiza majukumu ya mashirika na wananchi kuunga mkono kazi ya ujasusi chini ya sheria za China, lakini pia inasisitiza kazi ya ujasusi inapaswa kufuata sheria, kuheshimu na kulinda haki za binadamu, na kulinda maslahi ya watu binafsi na mashirika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako