• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Iran yasema ina haki ya kupinga makundi ya ugaidi nchini Pakistan kwa kuvuka mpaka

  (GMT+08:00) 2019-02-19 18:50:29

  Mnadhimu Mkuu wa jeshi la Iran Meja Jenerali Mohammad Bagheri amesema, Iran ina haki ya kuvuka mpaka na kuchukua hatua za kijeshi kama ikihitajika, ili kukomesha kambi za makundi ya ugaidi nchini Pakistan.

  Meja Jenerali Bagheri amesema, kama kambi hizo zikiendelea kutoa mafunzo na kuandikisha wapiganaji na kuwa maficho ya makundi ya ugaidi nchini Pakistan, Iran itachukua hatua za kijeshi moja kwa moja ikitakiwa kufanya hivyo.

  Amesema Iran inaitaka Pakistan iwajibike kupinga makundi ya ugaidi nchini humo au kuruhusu nguvu za kijeshi za Iran kuingia nchini Pakistan na kupambana na ugaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako