• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Rwanda yalenga dola milioni 88 kupitia kwa utalii wa mikutano

    (GMT+08:00) 2019-02-19 18:58:57

    Rwanda inalenga kukusanya dola milioni 88 kwa mwaka kupitia kwa utalii wa mikutano na maonyesho.

    Kituo cha mikutano nchini humo kinasema kuwa kinalenga kukusanya fedha hizo katika kipindi cha mwaka wa fedha cha 2019/2020.

    Mkurungezi wa kituo hicho Nelly Mukazayire amesema wana imani ya kufikia lengo hilo kwani tayari Rwanda imekuwa kituo muhimucha bishara na uwekezaji.

    Mwaka jana Rwanda ilipata dola milioni 52 kutokana na uandaaji wa mikutano ya kimataifa.

    Nelly amesema mwaka huu baadhi ya mikitano itakayofanyika nchini humo ni kama vile maonyesho ya kimataifa ya kahawa, mkutano wa usafiri wa anga na ule wa teknolojia barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako