• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Japan yatoa msaada wa miradi 3 Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-02-19 19:00:36

    Serikali ya Japan imetoa msaada wa Sh615 milioni kwa ajili miradi mitatu ya maendeleo katika sekta za elimu, maji na afya.

    Mkoa wa Kusini Pemba utapokea Sh288 milioni kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wavulana katika Shule ya Sekondari ya Juma Pindua, mkoa wa Mjini Magharibi utapokea Sh188 milioni kwa ajili ya usambazaji wa maji na mkoa wa Rukwa utapokea Sh139 milioni kwa ajili hospitali za Kirando na Mwimbi.

    Akizungumza wakati wa utiaji saini mkataba huo Balozi wa Japan nchini Tanzania, Shinichi Goto amesema walibaini kwamba kuna changamoto katika maeneo mbalimbali, hivyo wameamua kusaidia wananchi kupata huduma za afya na maji na wanafunzi kupata mabweni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako