• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • RIADHA: Huyu ndiye mtoto mwenye kasi zaidi, anatabiriwa kuvunja rekodi ya Usein Bolt

  (GMT+08:00) 2019-02-20 08:15:27

   

  Rudolph Ingram Jr maarufu kama 'Blaze' ni mtoto mwenye umri wa miaka saba na alianza kukimbia akiwa na miaka mitatu pekee baada ya kuangalia mashindano ya Olimpiki na babake.

  Blaze kwa sasa ndio mtoto mwenye kasi zaidi katika mchezo wa riadha, hii ni kutokana na kukimbia mbio za mita 100 kwa sekunde 13 tu na kuingia kwenye vitabu vya rekodi nchini Marekani kwa watu wenye umri wake.

  Wachambuzi wa riadha wanaamini Blaze ndiye mtu atakayekuja kuvunja rekodi iliyowekwa na mwanariadha mwenyekasi zaidi duniani Usein Bolt ambaye amewahi kukimbia mita 100 kwa 9.69 sekunde.

  Kwa mujibu wa baba mzazi wa mtoto huyo, Rudolph Ingram Sr ambaye ni kocha wa mchezo wa soka nchini Marekani amesema kuwa Blaze alianza kuvutiwa na riadha akiwa na miaka mitatu tu baada ya kutembelea mashindano ya Olimpiki

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako