• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mjumbe wa Umoja wa Mataifa azitaka pande zinazopambana za Yemen kufikia makubaliano ya kipindi cha pili cha kuondoa jeshi

  (GMT+08:00) 2019-02-20 18:29:34

  Mjumbe wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya Yemen Bw. Martin Griffiths amesema, tangu pande zinazopambana nchini Yemen zifikie makubaliano mwezi wa Desemba mwaka jana, hali nchini humo imekuwa na mabadiliko mazuri.

  Bw. Griffiths amesifu uratibu uliotolewa na viongozi wa pande hizo na kuzitaka kufikia makubaliano ya kipindi cha pili cha kuondoa jeshi.

  Naye naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya haki ya binadamu Bw. Mark Lowcock amesema, hivi sasa, hali ya haki ya binadamu nchini Yemen bado si nzuri, ambapo asilimia 80 ya Wayemen wanahitaji misaada. Ameongeza kuwa, watu milioni 20 hawapati huduma za afya na watu wengine milioni 18 hawana maji safi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako