• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Chama tawala nchini Uganda champitisha rais Museveni kugombea tena urais mwaka 2021

  (GMT+08:00) 2019-02-20 20:23:52

  Kamati Kuu ya chama tawala nchini Uganda NRM imetangaza kuwa, rais wa sasa wa nchi hiyo Yoweri Museveni atagombea tena nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2021.

  Taarifa iliyotolewa na chama hicho jana imesema, Kamati Kuu imetoa pendekezo kwa matawi mengine ya chama hicho kuwa, rais Museveni, ambaye amekuwa madarakani kwa zaidi ya miaka 30, aendelee kuongoza chama na nchi katika uchaguzi wa mwaka 2021 na zaidi.

  Kamati Kuu hiyo imefikia uamuzi huo baada ya majadiliano yaliyofanyika kwa wiki moja, wakati maofisa wa ngazi ya juu wa NRM walipojadili mambo kadhaa ikiwemo mwelekeo wa uchaguzi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako