• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yasukuma mbele mageuzi mapya vijijini

  (GMT+08:00) 2019-02-21 17:00:19

  Waziri wa kilimo na vijiji wa China Bw. Han Changfu amesema, mwaka jana China ilipata mafanikio mapya katika kuhimiza maendeleo ya kilimo na vijiji, na kupiga hatua imara katika juhudi za kupunguza umaskini, na huu ni mwanzo mzuri wa juhudi za kustawisha vijiji. Bw. Han ameongeza kuwa, kutokana na "mapendekezo kadhaa ya baraza la serikali la Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China kuhusu kazi za kilimo, vijiji na wakulima", China itasukuma mbele mageuzi mapya vijijini kwa kuanza na marekebisho ya sera ya ardhi, ili kuhimiza maendeleo vijijini.

  Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana, waziri wa kilimo na vijiji wa China Bw. Han Changfu amesema, mwaka jana maendeleo ya kilimo na vijiji nchini China yalikuwa na sura mpya. Anasema,

  "Mazao ya nafaka yalifikia karibu tani milioni 658, na kuzidi tani milioni 600 kwa miaka 7 mfululizo. Wakati huohuo mazao mengine yakiwemo nyama, mayai, maziwa, matunda, mboga na samaki yalitosheleza vizuri mahitaji ya watu. Aidha, kipato cha wakulima kiliongezeka kwa kasi, na wastani wa kipato cha watu walioko vijijini ulizidi dola 2,170 za kimarekani. Maendeleo ya vijiji yalikuwa na sura mpya."

  "Mapendekezo kadhaa ya baraza la serikali la Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China kuhusu kazi za kilimo, vijiji na wakulima" yaliyotolewa tarehe 19, yamedhihirisha majukumu muhimu ya kazi za kilimo, vijiji na wakulima kwa mwaka huu na mwakani, yakiwemo kupata ushindi katika vita dhidi ya umaskini, kuhakikisha usalama wa chakula, kuboresha mazingira ya makazi vijijini, na kusaidia wakulima kupata maisha bora. Bw. Han amesema uzalishaji wa chakula ni muhimu zaidi kati ya kazi za kilimo na vijiji, na pia ni tegemeo la China katika kukabiliana na changamoto ya uchumi na utatanishi wa aina mbalimbali. Anasema,

  "Mapendekezo ya mwaka huu ya baraza la serikali yamesisitiza umuhimu wa uzalishaji wa chakula, na kuagiza kuhakikisha utulivu wa sera na hatua za kilimo, na kushikilia mstari wa mwisho wa kudumisha mashamba hekta milioni 120 za kilimo."

  Bw. Han amesema kushughulikia vizuri uhusiano kati ya wakulima na ardhi ni mkazo wa kuhimiza mageuzi vijijini, na China itahimiza mageuzi hayo kwa kuanza na marekebisho ya sera ya ardhi.

  Aidha, Bw. Han amesema kipato cha mwakani cha wakulima kinatarajiwa kuongezeka na kuwa maradufu ya kile cha mwaka 2010. Anasema,

  "Katika miaka kadhaa iliyopita, kipato cha wakulima kimeongezeka kwa kasi. Mwaka huu na mwakani, China itaendelea kudumisha mwelekeo huu mzuri."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako