Kikosi cha usalama cha Iraq kimewakamata wapiganaji 24 wa kundi la IS walioingia kaskazini mwa nchi hiyo kutoka Syria.
Mnadhimu mkuu wa jeshi la serikali la Iraq Luteni Jenerali Othman al-Ghanmi amesema, wapiganji hao, wakiwemo vinara wanne wa ngazi ya juu wa kundi hilo waliingia jimbo la Ninewa. Pia ametoa amri kwa vikosi vya usalama kutekeleza kikamilifu hatua za usalama ili kuzuia kundi hilo kuingia jimbo la Mosul na maeneo mengine ya Ninewa.
Habari nyingine zinasema, jeshi la Iraq limeshambulia gari lililobeba wapiganaji wa kundi la IS katika kijiji cha Badoush na kuwaua wapiganaji watano.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |