Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeahidi kusaidia mkakati wa Maendeleo wa Jumuiya ya Afrika (EAC) ,ambao unahitaji $985 milioni katika kipindi cha miaka mitano.
Haya yaliafikiwa siku mbili zilizopita wakati Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Liberat Mfumukeko alikutana Rais wa Benki ya AfDB ,Dk Akinwumi A.Adesina katika makao makuu ya Benki hiyo jijini Abidjan Ivory Coast.
Mfumukeko aliomba msaada katika maeneo ya kilimo na viwanda,haswa viwanda vya kilimo.
Wakati wa mkutano huo Adesina alisema ni muhimu kuunganisha miradi ya miundombinu na maendeleo ya kilimo na viwanda kwa manufaa ya kuwa na uraia mmoja katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |