• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kikosi cha uhandisi cha kulinda amani cha China nchini Sudan Kusini chapita tathimini ya UNMISS

    (GMT+08:00) 2019-02-21 20:34:19

    Kikosi cha uhandisi cha kulinda amani cha China nchini Sudan Kusini kimepita tathimini ya uwezo wa kulinda amani iliyofanywa na Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, ikiwa ni mara ya kwanza kupata tathimini hiyo tangu kupangwa kwenye eneo hilo mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka jana.

    Kiongozi wa kikundi kinachofanya tathimini la UNMISS Cononeli Shahed amesema, askari wa China wana vifaa na silaha nzuri, nyaraka sahihi, na uwezo mzuri wa kitaaluma, na wanaamini kwamba wanaweza kukamilisha kazi mbalimbali zinazotolewa na UNMISS.

    Habari zinasema, tathimini hiyo inalenga kujua uwezo wa kivita wa vikosi mbalimbali, na ni njia muhimu ya kukagua kama vikosi vya kulinda amani vya maeneo tofauti vinaweza kutekeleza kazi yao kwa ufanisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako