• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Minara ya Kemboi na Vivian kuzinduliwa Mjini Eldoret

  (GMT+08:00) 2019-02-22 10:49:41

  Minara ya mabingwa wa riadha za dunia na mbio za Olimpiki, Ezekiel Kemboi na Vivian Cheruiyot itazinduliwa mjini Eldoret leo ikiwa ni siku moja kabla ya mashindano ya kitaifa ya mbio za nyika kuandaliwa katika uwanja wa Eldoret Sports Club.

  Minara hiyo ambayo imeandaliwa na hospitali ya Mediheal itazinduliwa katika makutano ya barabara ya Nairobi-Kapsabet na Kaptagat.

  Kemboi ameibuka mshindi wa Olimpiki katika mbio za mita 3,000 kuruka maji na viunzi mara mbili na kutawazwa mfalme wa dunia mara nne.

  Kwa upande wake, Cheruiyot alinyanyua nishani ya dhahabu katika mbio za mita 5,000 kwenye Olimpiki za Rio mnamo 2016.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako