• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kamati ya kusaidia Taifa Stars ifuzu AFCON 2019 yateuliwa

    (GMT+08:00) 2019-02-22 10:50:00
    Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imetaja Kamati maalum ya wajumbe 14 kwa ajili ya kuisaidia timu ya taifa, Taifa Stars ifuzu fainali za kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika kuanzia Juni 21 hadi Julai 19 mwaka huu nchini Misri.

    Taarifa hiyo ya TFF imeeleza kuwa kamati hiyo itaongozwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda atakayekuwa mwenyekiti na katibu ni Mhandisi Hersi Said.

    Jukumu kubwa la kamati hiyo ni kuhakikisha timu hiyo ya taifa inapata ushindi katika mchezo wake wa mwisho wa kundi L kuwania tiketi ya AFCON dhidi ya timu ya taifa ya Uganda (Uganda Crane) mechi itakayochezwa uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam Machi 22.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako