• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasukuma mbele mambo ya umma

    (GMT+08:00) 2019-02-22 19:04:17

    Wizara ya mambo ya umma ya China jana ilitoa ripoti ya mwaka jana kuhusu hali ya mageuzi na maendeleo ya mambo ya umma. Kutokana na ripoti hiyo, mwaka jana China ilisukuma mbele mambo ya umma kwa pande zote, na kupiga hatua katika kupunguza umaskini, na kuharakisha maendeleo ya huduma za wazee.

    Waziri wa mambo ya umma wa China Bw. Huang Shuxian amesema, mwaka jana wizara yake ilitoa mpango wa miaka mitatu wa kupunguza umaskini. Anasema,

    "Ruzuku kwa wakulima maskini katika wilaya zote zimefikia au kuzidi vigezo vya kitaifa katika kupunguza umaskini, na jumla ya watu milioni 18.12 wameandikishwa kupewa ruzuku hiyo. Mwaka jana, ruzuku za serikali kwa watu maskini mijini na vijijini zimeongezeka kwa asilimia 7.2 na 12.4 ikilinganishwa na mwaka 2017, na zaidi ya watu milioni 45 wamepata uhakikisho wa maisha ya kimsingi."

    Licha ya kupunguza umaskini, mwaka jana kazi nyingi muhimu ya wizara ya mambo ya umma ni kuharakisha maendeleo ya huduma za wazee. Naibu waziri wa wizara hiyo Bw. Gao Xiaobing amesema, katika miaka miwili iliyopita, wizara hiyo pamoja na idara nyingine husika zilifanya zoezi maalumu la kuboresha huduma katika vituo vya kutunza wazee. Anasema,

    "Mwaka 2017, tulirekebisha kasoro laki 1.97 za huduma, na mwaka jana tulirekebisha kasoro nyingine laki 1.63. Hadi sasa tumejenga vigezo vya kimsingi vya kutathmini huduma za mashirika ya kutunza wazee. Aidha mikoa 22 imezindua idara maalumu zinazoshughulikia usanifu wa huduma za wazee."

    Habari zinasema katika miaka miwili ijayo, wizara ya mambo ya umma itaanzisha mradi wa kuinua kiwango cha vituo vya kutunza wazee katika vijiji haswa vijiji maskini, na kutunga vigezo vya lazima kuhusu sifa na usalama wa mashirika ya kutunza wazee.

    Hivi karibuni, Kamati kuu ya Maendeleo na Mageuzi ya China ilitoa mpango wa kufungua soko la kutunza wazee. Bw. Gao amesema, wizara ya mambo ya umma itafanya vizuri kazi ya usimamizi. Anasema,

    "Baada ya kuondoa sera ya idhini ya kuanzisha mashirika ya kutunza wazee, kazi yetu imebadilika kutoka kutoa idhini na kuwa kufanya usimamizi. Usimamizi wetu kwa mashirika ya kiserikali au yasiyo ya kiserikali ni wazi, na pia tunatoa huduma kwa ajili ya mashirika hayo."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako