• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania yakiri kutenga milioni 612.8 kuendesha kesi dhidi ya kampuni ya madini

  (GMT+08:00) 2019-02-22 19:11:31

  Serikali ya Tanzania imekiri kuwa ilitenga zaidi ya Sh612.86 milioni miezi sita iliyopita kuendesha kesi iliyotokana na zuio la usafirishaji wa makinikia lililolitoa dhidi ya kampuni ya Acacia.

  Tanzania ilizuia usafirishaji wa mchanga wa madini uliokuwa unafanywa na kampuni hiyo mwaka 2017 jambo lililolalamikiwa na mchimbaji huyo kiasi ili kulinda masilahi yake.

  Ingawa mazungumzo bado yanaendelea baina ya Serikali na kampuni mama ya Barrick, kesi dhidi ya zuio hilo bado inaendelea na taarifa ya mabadiliko ya matumizi ya Serikali kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Julai hadi Desemba 2018 inaonyesha kutengwa kwa kiasi hicho.

  Katibu mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James amethibitisha kutolewa kwa fedha hizo. Kabla ya kuzuia usafirishaji wa mchanga wa madini, Serikali ilifanya uchunguzi kwa Rais John Pombe Magufuli kuunda kamati maalumu ambayo iligundua kampuni nyingi za uchimbaji madini hazijalipa kodi na ushuru mbalimbali unaotakiwa kwa muda mrefu.

  Kwenye orodha hiyo, Acacia ilikuwamo na ikatakiwa kulipa kodi na faini zake ambazo jumla yake ni Dola 190 bilioni (zaidi ya Sh418 trilioni). Hata hivyo, mazungumzo kati ya Serikali na Barrick bado yanaendelea kupata muafaka wa faini hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako