• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Idara ya usalama kupambana na wezi wa kahawa Kenya

  (GMT+08:00) 2019-02-22 19:11:48

  Vyombo vya usalama katika ukanda wa Mlima Kenya vimepanga kusambaratisha kabisa njama za wezi wa kahawa ambao huwasababishia wakulima hasara ya Sh3 bilioni kwa mwaka.

  Kwa mujibu wa mshirikishi wa usalama eneo hilo, Wilson Njega ambaye alizungumza na Radio China Kimataifa ni kuwa serikali imekuwa ikifanya udadisi wa hali hiyo ya wizi wa kahawa na kugundua kuwa huwa ni njama kati ya wasimamizi wa viwanda vya kahawa na wakora wengine katika mtandao wa biashara ya kahawa.

  Idara ya polisi imetoa onyo kali kwa wasimamizi wote wa viwanda kuwa ni laziwa wawe wakitoa maelezo kuhusu kiwango cha kahawa ambayo iko katika mabohari yao na siku ambayo inanuiwa kuwasilishwa hadi sokoni.

  Njega amesema kuwa baada ya kufahamishwa kuhusu kahawa katika stoo za viwanda hivyo, maafisa wa usalama watakuwa na uwezo wa kuweka mikakati ya kuilinda.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako